Treni ya Kuhakikishia: #KIKAOCHA MAZUNGUMZO 28 APRILI. TAFADHALI SEMA kwenye KingsChat Web
Devotional
TOFAUTISHA UKWELI NA MAMBO HALISI ~ PASTOR CHRIS OYAKHILOME
Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako? Ni nani atakayekaa katika mlima wako mtakatifu? Ni yeye aendaye kwa unyofu, na kutenda haki, na kusema kweli moyoni mwake (Zaburi 15:1-2).
Katika Yohana 8:32 Bwana Yesu alisema, "Nanyi mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru." Ukweli anaouzungumzia hapa ni ukweli katika ufalme wa Mungu, ambao ni tofauti na mambo halisi.
Kuna mambo halisi na kuna ukweli. Ukweli ni uhalisia, lakini si mambo yote halisi ni ya kweli. Jambo halisi linaweza kuwa ukweli, lakini linaweza lisiwe ukweli wa wakati wote. Kwa mfano, uchunguzi wa kimatibabu unaweza kuonyesha kwamba Mkristo ana uvimbe au maambukizi mwilini mwake; uchunguzi huo wa daktari ni jambo halisi, na si ukweli. Basi ukweli ni nini katika muktadha huu? Ukweli ni Neno la Mungu lililofunuliwa kuhusu afya yako kama Mkristo.
Uvimbe unaweza kuwa upo, lakini Neno la Mungu, ambalo ni UKWELI na uhalisia, linasema umefanywa mkamilifu katika Kristo (1 Petro 2:24). Ondoa macho yako kutoka kwenye mambo halisi ya kimwili na uweke umakini wako kwenye uhalisia wa Neno la Mungu, ambalo linathibitisha afya yako ya kimungu.
Hivyo ndivyo imani inavyofanya: inabadilisha mambo halisi kwa kukataa kuyapa umakini, kuzingatia au kutambua. Angalia maneno ya Mwalimu: Hakusema, "Mtaifahamu mambo halisi, nayo mambo halisi yatawaweka huru"; alisema "Mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru." Ukweli wa Neno la Mungu ndio unaokuokoa kutoka kwenye "mambo halisi" ya maisha. Kwa hiyo, unapaswa kuzingatia, na kusema tu, "ukweli," yaani, Neno la Mungu: "...neno lako ni kweli" (Yohana 17:17).
Aya yetu ya ufunguzi inazungumzia kusema ukweli moyoni mwako; unasemaje ukweli moyoni mwako? Inaanza kwa kufikiri ukweli moyoni mwako. Usipofikiri ukweli moyoni mwako hutausema ukweli.
Ukweli ni kile ambacho Mungu amesema kukuhusu katika Neno lake. Hicho ndicho kinachopaswa kuhesabiwa katika maisha yako; hicho ndicho kinachopaswa kutawala mawazo na maneno yako. Kwa mfano, mtu akikuambia, "Wewe si mwerevu sana; hakuna kitu maalum kukuhusu"; unapaswa kukataa mara moja na kujisemea ndani, "Ninajua mimi ni nani. Mimi ni hazina ya pekee ya Mungu, mwenye akili timamu, mwenye akili nyingi, na bora!"
MAOMBI
Baba mpendwa, nakushukuru kwa Neno lako, ukweli ambao ninaishi nao leo na kila siku. Neno lako limenipa mwanga na ufahamu, na limeimarisha imani yangu kushikilia yote uliyoyanipa katika Kristo Yesu. Ninaishi kwa ushindi, nikifanya njia yangu kuwa na mafanikio, ninapoishi ndani na kwa Neno lako, katika Jina la Yesu. Amina.
Salvation Prayer
O Lord God, I believe with all my heart in Jesus Christ, Son of the living God. I believe He died for me and God raised Him from the dead. I believe He's alive today.
I confess with my mouth that Jesus Christ is the Lord of my life from this day. Through Him and in His Name, I have eternal life; I'm born again.
Thank you Lord, for saving my soul! I'm now a child of God. Hallelujah!