Nguvu ya Sifa na Kuabudu
Devotional
NGUVU YA SIFA NA KUABUDU ~ PASTOR CHRIS OYAKHILOME.
Na mnamo usiku wa manane Paulo na Sila wakaomba, wakaimba nyimbo za kumsifu Mungu: na wafungwa wakawasikia. Mara kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata misingi ya gereza ikatikisika: na mara milango yote ikafunguka, na minyororo ya kila mmoja ikalegezwa (Matendo 16:25-26).
Matendo 16 inasimulia jinsi nyimbo za sifa kutoka kwa Paulo na Sila zilivyopelekea tetemeko la ardhi lililopangwa na Mungu ambalo lilipelekea kuachiliwa kwao kutoka kifungoni kibaya. Unapomsifu Bwana kutoka moyoni mwako katika uzuri wa utakatifu, matokeo ni mlipuko wa utukufu wa kiungu. Msifu na muabudu Bwana mbele ya changamoto za kutisha, na utukufu wake utaonekana kwa niaba yako.
Ikiwa unatamani muujiza leo, iwe ni katika kazi yako au fedha zako au hata matatizo kazini; au labda inahusiana na afya yako au ya mpendwa wako; chochote kile, kama kitendo cha imani, weka jambo hili mbele yako, na anza kuimba nyimbo za sifa katika roho na pia kwa kuelewa kwako tena na tena, kama roho inavyokupa maneno. Kwa kitendo hiki cha imani, unaitisha nguvu za Mungu mkuu—Mungu aliye juu zaidi—juu ya jambo lililo mbele yako.
Huna haja ya kusema mengi. Usizungumze kuhusu kitu kinachokusumbua; weka mtazamo wako kwa Bwana, unapoimba na kucheza kwa Bwana, ukiimba mistari ya sifa kumtukuza ukuu wake, nguvu za Mungu zitapita ndani yako. Usisimame wakati huu; kadri msukumo unavyoongezeka, zungumza kwa lugha tena na tena, mpaka upate noti ya ushindi.
Haijalishi hali ilivyo, ibada kama hiyo itafuatiwa na miujiza. Badala ya kuhisi huzuni, kutokuwa na msaada au kuzidiwa unapo kumbana na changamoto, tumia mkakati wa ibada na sifa; nguvu za Roho wa Mungu zitachochewa, na utakuwa na ushuhuda.
Salvation Prayer
O Lord God, I believe with all my heart in Jesus Christ, Son of the living God. I believe He died for me and God raised Him from the dead. I believe He's alive today.
I confess with my mouth that Jesus Christ is the Lord of my life from this day. Through Him and in His Name, I have eternal life; I'm born again.
Thank you Lord, for saving my soul! I'm now a child of God. Hallelujah!