Treni ya Uthibitisho: #UTHIBITISHOTRAIN 4 JULAI. Ninasema kwenye KingsChat Web
Devotional
PATA HABARI ZAKE ZA KARIBUNI – PASTOR CHRIS OYAKHILOME.
...Nilimtokea Abrahamu, Isaka, na Yakobo, kwa jina la Mungu Mwenyezi, lakini kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao (Kutoka 6:3).
Faida moja nzuri inayotokana na ushirika wa mara kwa mara na Bwana ni kwamba uko sawa na Roho; unapata habari mpya na za karibuni kutoka "makao makuu." Kupitia ushirika, tunapokea mawazo na mikakati kutoka kwa Baba; tunapata kuelewa zaidi, mambo anayotaka tufanye, na jinsi ya kuyafanya kulingana na viwango vyake, matakwa, na mapenzi yake kamilifu.
Unaweza kuwa unafanya kile ambacho Mungu alikuambia ufanye, lakini kama hauko katika ushirika wa mara kwa mara au mawasiliano na Yeye, unaweza kuwa unatekeleza jukumu lako bila "habari za karibuni za Baba." Unapotembea na Yeye, maarifa sahihi ya mapenzi yake, mipango yake, makusudi na nia zake yanakuwa wazi zaidi kwako.
Fikiria hivi: Ikiwa ulimwambia mtu akujengee nyumba, na akaja na muundo mzuri wa usanifu, kwa sababu nyumba ni yako, na unayo na unajua mpango mkuu, unaweza kuamua kufanya mabadiliko muhimu. Hata nyumba inapoendelea kujengwa, kila mara, kunaweza kuwa na kitu kipya unachotaka kuongeza. Unaona, maisha ni ya mabadiliko; miji yetu na jamii zetu ni za mabadiliko. Huwezi kusema, "Niliunda muundo miaka kumi iliyopita, na ndivyo itakavyobaki;" hapana! Kuna mabadiliko mengi na marekebisho yatakayohitajika unapokwenda mbele.
Maisha ya binadamu ni hivyo. Mungu anajenga Mwenyewe ndani yetu, na sisi ni vyombo vyake vya kujenga maisha yetu, na kujenga maisha ya wengine. Tunapaswa kuwa na ushirika na Yeye ili kuwa na habari za karibuni. Unahitaji habari zake za karibuni ili uweze kujenga kama anavyotaka.
Kwa mfano, ingawa Abrahamu, Isaka na Yakobo walimjua Mungu kama El Shaddai, Mungu alijitambulisha kwa Musa kama Yehova katika Kutoka 6. Wakati huo, Musa alikuwa na habari za karibuni. Lakini ufunuo umeendelea hata zaidi; hatuombi kwa Baba kwa jina "Yehova," wala hatufukuzi mapepo kwa jina la Yehova; tunatumia Jina la Yesu.
Hiyo ni habari za karibuni, tofauti na Yehova, El Shaddai au majina mengine ambayo Mungu alijitambulisha nayo katika Agano la Kale. Leo, Baba anajifunua katika Mwana wake, Yesu; Amejifunika ndani ya Yesu: "Kwa kuwa ilimpendeza Baba kwamba ndani yake ukae utimilifu wote" (Wakolosai 1:19).
MAOMBI
Baba mpendwa, nakushukuru, kwa kuwa Neno lako ni chanzo muhimu zaidi cha maarifa. Ninapojifunza Neno, roho yangu inajazwa na nuru kujua na kutembea katika mapenzi yako kamilifu daima, katika Jina la Yesu. Amina.
Salvation Prayer
O Lord God, I believe with all my heart in Jesus Christ, Son of the living God. I believe He died for me and God raised Him from the dead. I believe He's alive today.
I confess with my mouth that Jesus Christ is the Lord of my life from this day. Through Him and in His Name, I have eternal life; I'm born again.
Thank you Lord, for saving my soul! I'm now a child of God. Hallelujah!