Skip to main content

Jenga Maisha Yako Kwenye Ukweli

Devotional

JENGA MAISHA YAKO KWENYE UKWELI ~ MCHUNGAJI CHRIS OYAKHILOME.

Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu (Zaburi 119:105).

Wengi wamejenga maisha yao juu ya taarifa potofu, dhana na nadharia za wanadamu, badala ya Neno la Mungu. Tofauti na dunia hii na kila kitu kilichomo, unaweza kutegemea Neno; halikosei, na halibadiliki; Neno ni la milele, na lazima liwe chanzo cha taarifa unazoishi nazo.

Intaneti ambapo wengi hutafuta taarifa imeharibiwa na kuvamiwa na taarifa potofu ili kukuibia imani yako katika Biblia na Yesu Kristo. Wanaandika mambo dhidi ya Biblia, dhidi ya mambo ambayo Yesu alisema, dhidi ya mambo ambayo manabii walisema. Wanadai kupata utata katika Biblia na kwamba inahitaji kurekebishwa. Hawa ni watu walio na akili potofu na wadanganyifu ambao hawana Roho Mtakatifu!

Biblia ndiyo nyenzo pekee inayotegemewa duniani. Unaposimama mbele za Bwana, hatauliza kile mwalimu wako wa historia au profesa alikufundisha. Atauliza kuhusu Neno lake, kwa sababu taarifa zilizomo ziliandikwa kwa uvuvio wa Mungu.

Aya yetu ya ufunguzi inaelezea huduma ya Neno katika kukupa mwelekeo maishani. Haijalishi unachosikia au kusoma, fuata tu mwongozo na mwelekeo wa Neno. Jenga maisha yako juu ya ukweli wa Mungu.

OMBI

Baba mpendwa, asante kwa zawadi ya Maandiko. Nafungua moyo wangu na akili yangu kwa Neno lako, ili kuongozwa ninapojitoa kwa nguvu kuu ya Roho Mtakatifu leo. Ninapojifunza Neno kwa ufahamu wa kiroho, napokea ufahamu wa kina kuhusu yaliyopita, yaliyopo na yajayo ya mipango na makusudi yako kwa Kanisa, kwangu, na kwa dunia, na ninajengwa na kurushwa katika kiwango changu kingine cha mafanikio, ushindi na ustawi, katika Jina la Yesu. Amina.

Salvation Prayer

O Lord God, I believe with all my heart in Jesus Christ, Son of the living God. I believe He died for me and God raised Him from the dead. I believe He's alive today.

I confess with my mouth that Jesus Christ is the Lord of my life from this day. Through Him and in His Name, I have eternal life; I'm born again.

Thank you Lord, for saving my soul! I'm now a child of God. Hallelujah!

Follow Us

Follow Us